KIVUKO: Mwongozo wa kuendeshea warsha kuhusu VVU/UKIMWI, pamoja na mbinu za Mawasiliano, Mahusiano, Jinsia na Uhamasishaji

by Alice Welbourn

Petra Rohr-Rouendaal (Illustrator) and Adolf Mrema (Translator)

0 ratings • 0 reviews • 0 shelved
Book cover for KIVUKO

Bookhype may earn a small commission from qualifying purchases. Full disclosure.

Kivuko ni Mwongozo wa mafunzo wenye kitabu na mkanda wa video kuhusu VVU/UKIMWI, maswala ya jinsia na uhamasishaji, mbinu za mawasiliano na mahusiano. Kitabu hiki kimepewa kipaumbele kwa kuwa kinaeleza jinsi wanawake na vijana walivyo katika hatari kutokana na maamuzi wanayofanya kuhusu ngono. KIVUKO kimeundwa kuwasaidia wakufunzi na wanajamii kuendesha warsha ili kuwawezesha wanawake na wanaume kutafiti mahitaji yao ya kijamii, kingono na kisaikolojia; pia kusaidia kuchambua ugumu wa mawasiliano na kujizoesha njia mbalimbali za mawasiliano. Kwa ujumla warsha za Kivuko zinalenga kubadili tabia. Kitabu hiki kinaeleza jinsi ya kuendesha warsha na kina mazoezi mengi yanayohusisha maigizo mafupi pamoja na njia mbalimbali za kujifunza katika vikundi kwa kushirikiana. Vikundi vya warsha vimepangwa katika makundi manne tofauti ya rika kulingana na umri na jinsia. Picha za video ambazo zilichukuliwa Uganda, zimefanywa katika sehemu 15 fupi ambazo zimewekwa makusudi kuwarahisishia washiriki kujadiliana.
  • ISBN10 1905746253
  • ISBN13 9781905746255
  • Publish Date 31 March 2013
  • Publish Status Active
  • Publish Country GB
  • Imprint Strategies for Hope Trust
  • Format Paperback
  • Pages 246
  • Language swa