Tumeitwa Kuhudumia
1 primary work
Book 6
Kimetayarishwa Afrika ya Kusini Jimbo la Mashariki, kitabu hiki kinafafanua misingi mipya ya kuimarisha uthabiti kwa watoto ambao wamepitia huzuni na kufiwa. Kinawasaidia watu wazima ambao wanawahudumia watoto kuweza kugundua kwa upya na kuthamini 'undani wa mtoto' wa kwao wenyewe. Kitini cha TUMEITWA KUHUDUMIA kinajumuisha matendo, vijitabu vyenye kuhusisha matendo na miongozo midogo kuhusu mambo yanayohusu VVU na UKIMWI, vilivyoandaliwa kwa matumizi ya viongozi wa kanisa, hasa kwa nchi zilizo Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Madhumuni ya mambo yaliyomo ni kuwawezesha wachungaji, mapadre, watawa wa kike na wa kiume, walei viongozi wa kanisa na waumini wao pamoja na jamii ili waweze: - Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ya janga la VVU na wito wa Kikristo wa kuitikia kwa huruma. - Kushinda unyanyapaa, ukimya, ubaguzi, kukataa, woga na kukataa kubadilika, hali ambazo zinazuia kanisa na jamii katika kukabiliana na mambo yanayohusu VVU na UKIMWI kwa ukamilifu zaidi.
- Kuwaongoza waumini wao na jamii katika mchakato wa kujifunza na kubadilika kutakakopelekea kwenye matendo na mienendo ya kikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ili kupunguza kuenea kwa VVU na kupunguza athari za janga la VVU. TUMEITWA KUHUDUMIA ni wazo la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini, ambao wanatayarisha na kutoa vitabu na video vinavyohamasisha mbinu madhubuti na michakato ya kijamii ya kuhudumia, kusaidia na kuzuia VVU na UKIMWI katika nchi zinazoendelea duniani, hasa zilizoko Afrika chini ya Jangwa la Sahara. TUMEITWA KUHUDUMIA inatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, shirikisho la muungano wa makanisa, na taasisi nyingine za kidini, miundo ya kimataifa ya makanisa, wachapishaji, wasambazaji na washika dau wengine.